Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitufunza Istikhaarah katika mambo yote kama anavyotufunza Suurah katika Qur-aan. Amesema: ”Mmoja wenu anapotaka kufanya jambo basi aswali Rak´ah mbili mbali na Swalah ya faradhi na kisha aseme:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْتَخيرُكَ بِعِلْمِكَ وأَسْتَقْدِرُكَ بقدرَتِكَ وأَسْأَلُكَ منْ فَضْلِكَ الْعَظِيمِ فَإِنَّكَ تَقْدِرُ وَلاَ أَقْدِرُ وَتَعْلَمُ وَلاَ أَعْلَمُ وَأَنْتَ عَلاَّمُ الْغُيُوبِ اللهُمَّ إِنْ كُنتَ تَعلم أَنَّ هذَا الأَمْرَ خيرٌ لِي في دِيني وَمَعَاشي وَعاقِبة أَمْرِي وَعَاجِلِهِ وَآجِلِهِ فاقْدُرْهُ لِي وَيَسِّرْهُ لي ثمَّ بَارِكْ لي فيهِ وَإِنْ كُنْتَ تَعْلَم أَنَّ هَذا الأَمْرَ شَرٌّ لِي في دِينِي وَمَعَاشِي وَعَاقِبَةِ أَمْرِي وَعَاجِلِهِ وَآجِلِهِ فاصْرِفْهُ عَنِّي واصرفْنِي عَنْهُ واقْدُرْ لِيَ الْخَيْرَ حَيْثُ كانَ ثم رضِّنِي بهِ

“Ee Allaah! Hakika mimi ninakutaka kwa ujuzi Wako na ninakumba uniwezeshe kwa uwezo Wako. Ninakuomba kwa fadhila Zako kubwa. Hakika Wewe unaweza na mimi siwezi. Wewe unajua na mimi sijui. Wewe ni Mjuzi wa yale yaliyofichikana. Ee Allaah! Endapo unajua kuwa jambo hili – litaje jambo lako – ni kheri kwangu katika Dini yangu, mwisho wa maisha yangu duniani na Aakhirah, basi nakuomba uniwezeshe na unisahilishie, kisha nibariki kwalo. Na endapo unajua kuwa jambo hili ni shari kwangu katika dini yangu, mwisho wa maisha yangu duniani na Aakhirah, basi nakuomba liepushe na mimi na mimi uniepushe nalo, na nipangie jambo jengine lenye kheri na mimi popote lilipo, halafu niridhishe kwalo.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy.

Sa´d bin Abiy Waqqaas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Miongoni mwa furaha ya mwanadamu ni kumuomba Allaah amchagulie, na miongoni mwa furaha ya mwanadamu ni kuridhia aliloliamua Allaah. Miongoni mwa maangamizi ya mwanadamu ni kuacha kumuomba Allaah amchagulie, na miongoni mwa maangamizi ya mwanadamu ni kuchukizwa na aliloamua Allaah.”[2]

Ameipokea Ahmad.

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Hajawahi kujuta yule aliyemuomba Allaah amchagulie jambo lake, akashauriana na viumbe na akawa na msimamo juu ya jambo lake. Allaah (Ta´ala) amesema:

أَلَمْ تَرَ أَنَّهُمْ فِي كُلِّ وَادٍ يَهِيمُونَ

”Je, huoni kuwa wao katika kila bonde wanatangatanga?”[3]

Qataadah amesema:

”Hawakuwahi watu kushauriana kwa ajili ya kutafuta radhi za Allaah isipokuwa waliuonyeshwa njia ya sawasawa katika jambo lao.”[4]

[1] al-Bukhaariy (1162, 6382 na 7390).

[2] Ahmad (1/459), at-Tirmidhiy (2151), aliyesema kuwa ni ngeni, na al-Bazzaar (4/18-19). Cheni yake ya wapokezi ni dhaifu kwa mujibu wa Ahmad Shaakir na dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (2151).

[3] 3:159

[4] al-Kalim at-Twayyib, uk. 116

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 293-294
  • Imechapishwa: 08/09/2025