Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika Allaah anapenda kupiga chafya na anachukia kwenda miayo. Mmoja wenu anapopiga chafya na kumhimidi Allaah, basi kila anayemsikia aseme:
يَرْحَمُكَ الله
”Allaah akurehemu.”
Ama kupiga miayo kunatokana na shaytwaan. Basi mmoja wenu anapopiga miayo ajizuilie kadiri awezavyo. Kwani mmoja anapoenda miayo basi shaytwaan humcheka.”[1]
Ameipokea al-Bukhariy.
Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Anapochemua mmoja wenu, basi aseme:
الْحَمْـدُ للهِ
“Himdi zote ni stahiki ya Allaah.”
Ndugu au rafiki yake amwambie:
يَرْحَمُـكَ الله
“Allaah akurehemu.”
Atakapoambiwa hivo basi aseme tena:
يَهْـديكُـمُ اللهُ وَيُصْـلِحُ بالَـكُم
“Allaah awaongoze na ayatengeneze mambo yenu.”[2]
Ameipokea al-Bukhariy.
Imekuja katika tamko la Abu Daawuud:
الْحَمْدُ للهِ عَلى كُلِّ حَال
”Himdi zote njema anastahiki Allaah kwa kila hali.”
Abu Muusa al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mmoja wenu akipiga chafya na kumhimidi Allaah, basi muombeeni rehema. Asipomhimidi Allaah, basi msimwombee rehema.”[3]
Ameipokea Muslim.
[1] al-Bukhaariy (3289, 6223 na 6226).
[2] al-Bukhaariy (6224).
[3] Muslim (2992).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 347-348
- Imechapishwa: 15/09/2025
Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika Allaah anapenda kupiga chafya na anachukia kwenda miayo. Mmoja wenu anapopiga chafya na kumhimidi Allaah, basi kila anayemsikia aseme:
يَرْحَمُكَ الله
”Allaah akurehemu.”
Ama kupiga miayo kunatokana na shaytwaan. Basi mmoja wenu anapopiga miayo ajizuilie kadiri awezavyo. Kwani mmoja anapoenda miayo basi shaytwaan humcheka.”[1]
Ameipokea al-Bukhariy.
Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Anapochemua mmoja wenu, basi aseme:
الْحَمْـدُ للهِ
“Himdi zote ni stahiki ya Allaah.”
Ndugu au rafiki yake amwambie:
يَرْحَمُـكَ الله
“Allaah akurehemu.”
Atakapoambiwa hivo basi aseme tena:
يَهْـديكُـمُ اللهُ وَيُصْـلِحُ بالَـكُم
“Allaah awaongoze na ayatengeneze mambo yenu.”[2]
Ameipokea al-Bukhariy.
Imekuja katika tamko la Abu Daawuud:
الْحَمْدُ للهِ عَلى كُلِّ حَال
”Himdi zote njema anastahiki Allaah kwa kila hali.”
Abu Muusa al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mmoja wenu akipiga chafya na kumhimidi Allaah, basi muombeeni rehema. Asipomhimidi Allaah, basi msimwombee rehema.”[3]
Ameipokea Muslim.
[1] al-Bukhaariy (3289, 6223 na 6226).
[2] al-Bukhaariy (6224).
[3] Muslim (2992).
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 347-348
Imechapishwa: 15/09/2025
https://firqatunnajia.com/unapochemua-na-kupiga-miayo-2/