´Abdullaah bin Busr (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifikia kwa baba yangu. Tukamletea chakula na kinywaji. Basi baba yangu akamwambia: ”Tuombee kwa Allaah.” Ndipo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

اللهُمَّ بَارِك لهم فيما رَزَقْتهم واغْفِرْ لَهُمْ وارْحَمْهُمْ

“Ee Allaah! Wabariki katika ulichowaruzuku, uwasamehe na uwarehemu.”[1]

Ameipokea Muslim.

Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alialikwa kwa Sa´d bin ´Ubaadah ambapo akaletewa mkate na mafuta ya mzeituni akala. Kisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

أَفْطرَ عِنْدَكُم الصَّائِمُونَ وَأَكَلَ طَعَامَكُمْ الأَبْرَارُ وَصَلَّتْ عَلَيْكُم الملائِكَةُ

”Wafuturu kwenu waliofunga. Wale chakula chenu waliowema. Malaika wakuombeeni du´aa.”[2]

 Ameipokea Daawuud.

Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Abul-Haytham bin at-Twayyihaan alimtengenezea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) chakula ambapo akamkaribisha nacho Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake. Walipomaliza akasema: ”Mlipe malipo ndugu yenu.” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Tunamlipaje?” Akasema: “Hakika mtu anapoingia nyumbani mwa mtu, akala chakula na kunywa kinywaji chake, basi amwombee du´aa. Huko ndio kumlipa kwake.”[3]

Ameipokea Abu Daawuud.

[1] Muslim (2042).

[2] Abu Daawuud (3854) na Ahmad (4/356-357). Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib” (152).

[3] Abu Daawuud (3853). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (3853).

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 342-343
  • Imechapishwa: 23/09/2025