Unapata thawabu zake hata kama hakushiba

Swali: Ambaye anasema:

“Mwenye kumfuturisha mwenye kufunga ana mfano wa ujira wake pasi na kupungua chochote kwenye ujira wa mfungaji.”

kwamba ni lazima ashibe. Nini maoni yako juu ya jambo hili?

Jibu: Hapana, Hadiyth zinajulisha kuwa si lazima kushibisha.

Swali: Je, thawabu zinapatikana bila kushiba?

Jibu: Ndio, hata kama hakushiba.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25189/هل-يلزم-الاشباع-في-اجر-من-فطر-صاىما
  • Imechapishwa: 14/02/2025