Swali: Je, watu watafufuliwa siku ya Qiyaamah wakiwa katika umri wa meno waliokufa nao?
Jibu: Watu watafufuliwa siku ya Qiyaamah, kama alivyotueleza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wakiwa hawana viatu, wakiwa uchi na wakiwa hawajatahiriwa. Maana ya “hawana viatu” ni kwamba hawatakuwa na viatu. Na “wakiwa uchi” ni kwamba hawatakuwa na nguo. Na “wakiwa hawajatahiriwa” ni kwamba hawatakuwa wametahiriwa, kama walivyozaliwa na mama zao. Kila mtu atakuwa akitazama kuelekea mbinguni. Hakuna mtu atakayemjali mwingine wala kumtazama mwingine kutokana na ukubwa wa khofu na balaa hilo. Waumini watakapoingia Peponi – tunamuomba Allaah atujaalie sisi na nyinyi tuwe miongoni mwao – watakuwa vijana wenye umri wa miaka thelathini na mitatu.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
- Imechapishwa: 30/09/2026
Swali: Je, watu watafufuliwa siku ya Qiyaamah wakiwa katika umri wa meno waliokufa nao?
Jibu: Watu watafufuliwa siku ya Qiyaamah, kama alivyotueleza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wakiwa hawana viatu, wakiwa uchi na wakiwa hawajatahiriwa. Maana ya “hawana viatu” ni kwamba hawatakuwa na viatu. Na “wakiwa uchi” ni kwamba hawatakuwa na nguo. Na “wakiwa hawajatahiriwa” ni kwamba hawatakuwa wametahiriwa, kama walivyozaliwa na mama zao. Kila mtu atakuwa akitazama kuelekea mbinguni. Hakuna mtu atakayemjali mwingine wala kumtazama mwingine kutokana na ukubwa wa khofu na balaa hilo. Waumini watakapoingia Peponi – tunamuomba Allaah atujaalie sisi na nyinyi tuwe miongoni mwao – watakuwa vijana wenye umri wa miaka thelathini na mitatu.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
Imechapishwa: 30/09/2026
https://firqatunnajia.com/umri-wa-watu-watapofufuliwa-siku-ya-qiyaamah/