Ni ipi Tabarruk inayokubalika katika Shari´ah?

Swali: Ni ipi Tabarruk inayokubalika katika Shari´ah? Ni ipi Tabarruk iliyo haramu?

Jibu: Haifanywi Tabarruk kwa chochote katika njia za shirki, kama vile mawe na mfano wake. Vivyo hivyo kufanya Tabarruk kwa Ka´bah. Yote haya ni katika Bid´ah.

Ama Tabarruk inayokubalika katika Shari´ah ni kuomba baraka kutoka kwa Allaah kwa mfano kwa kujifunza elimu, kuwauliza wanazuoni huku akitarajia baraka na faida kutoka kwa Allaah, kutarajia baraka kutoka kwenye maji ya zamzam kwa kunywa na kumuomba Allaah ajaalie yawe na baraka.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
  • Imechapishwa: 30/09/2026