Swali: Mtu amesahau kufanya Twawaaf-ul-Ifaadhwah na akakumbuka baada ya kufika nyumbani kwake na kwa sasa hawezi kurudi. Kipi kinachompasa?
Jibu: Ni lazima arudi, kwa sababu Twawaaf ni nguzo miongoni mwa nguzo za Hajj. Kwa hivyo ni lazima arudi kuitekeleza. Amekatazwa kumjamii mke wake. Ikiwa atamwingilia, ikiwa alikuwa amefanya Tahallul ya kwanza, basi kwa mujibu wa wanazuoni analazimika kutoa fidia ya damu. Vilevile analazimika kwenda kufanya Twawaaf-ul-Ifaadhwah. Lakini ikiwa hajafanya Tahallul ya kwanza, basi Hajj yake imeharibika. Kinachokusudiwa ni kwamba ni lazima aitekeleze Twawaaf hiyo na ni lazima arudi mara moja, kwa sababu ni nguzo miongoni mwa nguzo za Hajj ambayo haidondoki kwa sababu ya kutojua, kusahau, kwa makusudi wala kwa udhuru wowote kati ya udhuru huo.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
- Imechapishwa: 30/09/2026
Swali: Mtu amesahau kufanya Twawaaf-ul-Ifaadhwah na akakumbuka baada ya kufika nyumbani kwake na kwa sasa hawezi kurudi. Kipi kinachompasa?
Jibu: Ni lazima arudi, kwa sababu Twawaaf ni nguzo miongoni mwa nguzo za Hajj. Kwa hivyo ni lazima arudi kuitekeleza. Amekatazwa kumjamii mke wake. Ikiwa atamwingilia, ikiwa alikuwa amefanya Tahallul ya kwanza, basi kwa mujibu wa wanazuoni analazimika kutoa fidia ya damu. Vilevile analazimika kwenda kufanya Twawaaf-ul-Ifaadhwah. Lakini ikiwa hajafanya Tahallul ya kwanza, basi Hajj yake imeharibika. Kinachokusudiwa ni kwamba ni lazima aitekeleze Twawaaf hiyo na ni lazima arudi mara moja, kwa sababu ni nguzo miongoni mwa nguzo za Hajj ambayo haidondoki kwa sababu ya kutojua, kusahau, kwa makusudi wala kwa udhuru wowote kati ya udhuru huo.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
Imechapishwa: 30/09/2026
https://firqatunnajia.com/amesahau-twawaaf-ul-ifaadhwah/