Umeme umerudi punde tu baada ya kumaliza kutoa adhaana

Swali: Muadhini akiadhini bila ya kipaza sauti kwa sababu ya kukatika umeme kisha punde tu baada ya adhaana umeme ukaja. Je, airudhie adhaana kwenye kipaza sauti au atosheke na adhaana yake ya kwanza?

Jibu: Atosheke na ile adhaana yake ya kwanza. Hapana haja ya kuirudia, kwa sababu watu wameshasikia adhaana kutoka misikiti mingine pembezoni mwake. Lakini ikiwa ndio msikiti pekee na hakuna misikiti mingine pembezoni mwake, hapo anaweza kuirudia ili watu wajue kuwa umeingia wakati wa swalah.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/198)
  • Imechapishwa: 11/04/2026