Swali: Mimi niko katika masomo ya kuhifadhi Qur-aan tukufu. Kwa mfano tunapangiwa juzu tano. Lakini huenda wakati mwingine mwalimu akawapunguzia silebasi wale wanafunzi na akawapa chini ya silebasi hiyo. Inajuzu kwa mwalimu kufanya hivo?
Jibu: Haifai kwa mwalimu kupunguza wala kugeuza kitu katika silebasi. Kwa sababu ameaminiwa. Ameaminiwa pande mbili; nchi imemwamini na wanafunzi pia wamemwamini. Ameaminiwa baina ya wanafunzi na wazazi wao. Ni lazima kwake kufuata ule utaratibu. Lakini wakati fulani ile silebasi inakuwa kubwa kuliko wakati na hapo ndipo kunatokea matatizo. Kwa mfano silebasi inakuwa juzu tano na wakati alopewa hautoshi kufundisha juzu tano. Mwalimu achukue msimamo gani? Katika hali hii naona kuwa waalimu wanatakiwa kuiandikia cheti idara ya masomo, idara ya masomo wao wataiandikia idara ya mafunzo na idara ya mafunzo wataiandikia wizara na kuwaeleza kwamba wakati tulopewa hautoshi kufundisha silebasi hii na hivyo waongeze muda kuliko kufundisha mada tatu badala ya mbili.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (58) http://binothaimeen.net/content/1325
- Imechapishwa: 05/11/2019
Swali: Mimi niko katika masomo ya kuhifadhi Qur-aan tukufu. Kwa mfano tunapangiwa juzu tano. Lakini huenda wakati mwingine mwalimu akawapunguzia silebasi wale wanafunzi na akawapa chini ya silebasi hiyo. Inajuzu kwa mwalimu kufanya hivo?
Jibu: Haifai kwa mwalimu kupunguza wala kugeuza kitu katika silebasi. Kwa sababu ameaminiwa. Ameaminiwa pande mbili; nchi imemwamini na wanafunzi pia wamemwamini. Ameaminiwa baina ya wanafunzi na wazazi wao. Ni lazima kwake kufuata ule utaratibu. Lakini wakati fulani ile silebasi inakuwa kubwa kuliko wakati na hapo ndipo kunatokea matatizo. Kwa mfano silebasi inakuwa juzu tano na wakati alopewa hautoshi kufundisha juzu tano. Mwalimu achukue msimamo gani? Katika hali hii naona kuwa waalimu wanatakiwa kuiandikia cheti idara ya masomo, idara ya masomo wao wataiandikia idara ya mafunzo na idara ya mafunzo wataiandikia wizara na kuwaeleza kwamba wakati tulopewa hautoshi kufundisha silebasi hii na hivyo waongeze muda kuliko kufundisha mada tatu badala ya mbili.
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (58) http://binothaimeen.net/content/1325
Imechapishwa: 05/11/2019
https://firqatunnajia.com/ulazima-kwa-waalimu-kufuata-silebasi-ya-masomo/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)