Swali: Ni lini ukarimu unakuwa wenye kusimangwa?

Jibu: Pale anapoweka pasi po mahali pake kwa namna ya kwamba akampa mtu ambaye anajisaidia kufanya maasi, akawapa wapumbavu wakacheza kwa pesa hizo, ukarimu pasi po mahali pake kama vile katika kununua yale aliyoharamisha Allaah au katika kuharibu pesa. Ukarimu unatakiwa kuwekwa mahali pake kama vile kuwapa wahitaji, mafukara na masikini, kuanzisha miradi ya hisani, kuwalipia watu madeni yao, kujitolea mali katika kupambana katika njia ya Allaah, kuwakomboa watumwa na mfano wa hayo ambayo yanasifiwa kwa mujibu wa Shari´ah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24183/ما-الاحوال-التي-يكون-الجود-مذموما
  • Imechapishwa: 13/09/2024