Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

188 – Mama wa waumini Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

(إنَّهُ يُسْتَعْمَلُ عَلَيْكُمْ أُمَرَاءُ فَتَعرِفُونَ وتُنْكِرُونَ، فَمَنْ كَرِهَ فَقَدْ بَرِئَ، وَمَنْ أنْكَرَ فَقَدْ سَلِمَ، وَلَكِنْ مَنْ رَضِيَ وَتَابَعَ)

.قَالوا: يَا رَسُول اللهِ، ألا نُقَاتِلهم؟ قَالَ: (لا، مَا أَقَامُوا فيكُمُ الصَّلاةَ)

“Mtaletewa watawala ambao kuna mambo mtayoyajua na mengine mtayachukia; yule atakayechukia basi ameokoka, na yule atakayekanya amesalimika, lakini yule atakayeridhia na kufuata [basi huyo ataangamia kama watavyoangamia].” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah, si tumpige vita?” Akasema: “Hapana, maadamu anasimamisha swalah.”[1]

Katika Hadiyth hii kuna dalili yenye kuonyesha kuwa kuacha swalah ni kufuru. Hilo ni kwa sababu haijuzu kuwapiga vita watawala isipokuwa pale tutapoona kufuru ya wazi ambayo tuna dalili kwayo kutoka kwa Allaah. Ikiwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameturuhusu kuwapiga vita pale ambapo hawaswali, hiyo ni dalili yenye kuonyesha kwamba kuacha swalah ni kufuru ya wazi ambayo tuna dalili kwayo kutoka kwa Allaah.

Hii ndio maoni ya haki. Yule mwenye kuacha swalah kabisa, haswali na mkusanyiko wala nyumbani kwake, ni kafiri mwenye kufuru yenye kumtoa katika Uislamu.

Haikupokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kuwa mwenye kuacha swalah ataingia Peponi, ni muumini, ameokolewa na Moto au mfano wa hayo.

Lililo la wajibu ni kuyapitisha maandiko kama yalivokuja juu ya kufuru ya mwenye kuacha swalah. Kila ambaye alikuja na hoja kuonyesha kuwa hakufuru, ni hoja isiyomfaa. Kwa sababu itakuwa inaingia katika moja ya mafungu yafuatayo:

1 – Ima msingi hakuna dalili.

2 – Imefungwa na sifa ambazo haingii humo mwenye kuacha swalah.

3 – Imefungwa na hali ambapo mwenye kuacha swalah anapewa udhuru.

4 – Ni yenye kuenea na imekhusishwa na maandiko ya kufuru ya mwenye kuacha swalah.

5 – Au ni dhaifu.

Dalili za mwenye kusema ya kwamba mwenye kuacha swalah hakufuru kabisa hazitoki nje ya mafungu haya matano.

Maoni ya sawa kwangu ni kwamba mwenye kuacha swalah ni kafiri kufuru yenye kumtoa katika Uislamu na ukafiri wake ni mbaya zaidi kuliko wa mayahudi na manaswara. Mayahudi na manaswara wanakubaliwa na dini zao. Kuhusu yeye hakubaliwi. Kwa kuwa anahesabika ni mwenye kuritadi. Anatakiwa kuambiwa atubu na la sivyo auawe.

[1]Muslim (1854).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (27)
  • Imechapishwa: 18/08/2025