Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
35 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Msihusudiane, msifanyiane hadaa, msichukiane… “
Kuchukiana inahusu mambo yote ambayo inaweza kuwa ni sababu ya kutokea chuki, sawa ikiwa ni katika maneno na matendo. Kila neno ambalo linapelekea katika kuleta chuki umekatazwa nalo. Kila kitendo ambacho kinapelekea katika kuleta chuki umekatazwa nacho.
Muumini ameamrishwa kujitahidi kufanya mambo yanayoleta mapenzi kati ya ndugu zake waislamu. Kuhusiana na kufanya mambo ambayo yanapelekea katika kuleta chuki, ni haramu akajaribu kuyafanya sawa ikiwa ni kwa njia ya maneno, matendo, mwenendo, ishara au hatua zake.
Haifai kwa muislamu kumchukia muislamu yoyote. Kwa sababu anaweza kumpenda kutokana na yale aliyomo katika Uislamu na Tawhiyd. Haya yanafunika mengine.
Ama akimchukia chuki kwa ajili ya Allaah ni sawa. Hapa inahusiana na chuki za kidunia. Ndio ambayo tumekatazwa hapa.
- Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 482-483
- Imechapishwa: 12/05/2020
Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
35 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Msihusudiane, msifanyiane hadaa, msichukiane… ”
Kuchukiana inahusu mambo yote ambayo inaweza kuwa ni sababu ya kutokea chuki, sawa ikiwa ni katika maneno na matendo. Kila neno ambalo linapelekea katika kuleta chuki umekatazwa nalo. Kila kitendo ambacho kinapelekea katika kuleta chuki umekatazwa nacho.
Muumini ameamrishwa kujitahidi kufanya mambo yanayoleta mapenzi kati ya ndugu zake waislamu. Kuhusiana na kufanya mambo ambayo yanapelekea katika kuleta chuki, ni haramu akajaribu kuyafanya sawa ikiwa ni kwa njia ya maneno, matendo, mwenendo, ishara au hatua zake.
Haifai kwa muislamu kumchukia muislamu yoyote. Kwa sababu anaweza kumpenda kutokana na yale aliyomo katika Uislamu na Tawhiyd. Haya yanafunika mengine.
Ama akimchukia chuki kwa ajili ya Allaah ni sawa. Hapa inahusiana na chuki za kidunia. Ndio ambayo tumekatazwa hapa.
Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 482-483
Imechapishwa: 12/05/2020
https://firqatunnajia.com/uharamu-wa-waislamu-kuchukiana/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)