Napendekeza vitabu kama ”Waqafaat ma´ Kitaab ’Lid-Du´aati faqatw” na ”at-Twariyq ilaa al-Jamaa´ah al-Umm”. Vinahusu mfumo. Sisi hatuvutani na al-Ikhwaan al-Musllimuun kwa sababu wananyoa ndevu au wanavaa suruwali, wanaokula mirungi au kuvuta sigara. Hapana. Katika jamii wako ambao ni waovu zaidi kuliko wao. Ugomvi wetu nao ni kutokana na uharibifu wa mfumo wao. Ni wenye kiu juu ya utawala. Sio watu wa ulinganizi. Wangelikuwa ni watu wa ulinganizi, basi wasingeliwatupilia mbali Ahl-us-Sunnah na wakaenda kupatana na Suufiyyah, Shiy´ah, chama cha Ahraar, ambacho ni miongoni mwa vile vyama kumi vilivyofanya makubaliano. Tumeosha mikono yetu kutokana na watu hawa ingawa wanasapotiwa na watu wema.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 427
  • Imechapishwa: 18/07/2025