Swali: Je, inajuzu kuwasifu Ahl-ul-Kitaab wote kwamba ni watu waaminifu kutokana na maneno Yake (Ta´ala):

وَمِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مَنْ إِن تَأْمَنْهُ بِقِنطَارٍ يُؤَدِّهِ إِلَيْكَ

“Na miongoni mwa Ahl-ul-Kitaab yuko ambaye ukimpa amana ya mrundi wa mali atakurejeshea”? (03:75)

Jibu: Ueneaji huu umeutoa wapi? Aayah hii inahusiana na Ahl-ul-Kitaab maalum na si wote.

وَمِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ

“Na miongoni mwa Ahl-ul-Kitaab… “

Bi maana baadhi ya Ahl-ul-Kitaab. Wewe soma matamshi ya Aayah tu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13965
  • Imechapishwa: 26/06/2020