Swali: Sisi ni familia ambao tunaishi katika nyumba moja na baba yetu hakutugawanyia. Wawili katika sisi wanapokea mshahara, lakini katika ´Iyd-ul-Adhwhaa tunachinja mnyama mmoja tu. Je, mnyama huyo anatutosha sote?

Jibu: Ndio, mkiwa katika nyumba moja na mnashirikiana katika jengo hilo ambapo chakula chenu ni kimoja, kinakutosheni kichinjwa kimoja. Lakini ikiwa nyumba ina ghorofa tofauti na kila mmoja yuko katika ghorofa yake ya kujitegemea, basi Sunnah ni kwa kila watu wa ghorofa yao au kila watu kwa chumba chao wachinje kivyao. Hiyo ndio Sunnah. Lakini mkiwa mmekusanyika ambapo hali yenu ni moja, chakula chenu ni kimoja ambapo mnashirikiana katika nyumba – ni mamoja jengo moja au majengo mengi – kichinjwa kimoja kinatosha. Hapana vibaya endapo mtachinja vichinjwa vingi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/18330/هل-تجزى-الاضحية-الواحدة-عن-العاىلة
  • Imechapishwa: 12/06/2024