Udanganyifu kwa mwanamke kuvaa suruwali

Swali: Ni ipi hukumu kwa mama au wasichana kuvaa suruwali?

Jibu: Msiwazoeze wasichana wadogo kuvaa suruwali. Suruwali inabana. Haisitiri. Ikiwa inasitiri ngozi, haisitiri maumbile. Pengine ikampamba mwanamke zaidi. Fitina katika kuvaa suruwali ni kubwa kuliko kutoivaa. Fitina yake ni kubwa. Kwa kuwa inatoa picha kinyume na uhakika wake. Pengine mwanamke akawa mbaya na asiyetamanika, lakini pale ambapo anavaa suruwali na ikaonesha maumbile yake, wanaume wakadanganyika naye. Wakati angelijua yale yaliyochini yake, asingelimtamani.

Check Also

Kuweka kompyuta na intaneti nyumbani

Swali: Ni ipi hukumu ya kuweka intaneti nyumbani, ni mamoja ikiwa kwa haja au bila …