Tofauti kati ya du´aa ya ´ibaadah na du´aa ya maombi

Swali: Ni ipi tofauti kati ya du´aa ya ´ibaadah na du´aa ya maombi?

Jibu: Du´aa ya ´ibaadah ni matendo mema; husemwa kuwa ni du´aa ya ´ibaadah. Swalah ni du´aa ya ´ibaadah, swawm ni du´aa ya ´ibaadah, swadaqah ni du´aa ya ´ibaadah, Tasbiyh na Tahliyl ni du´aa ya ´ibaadah. Kwa sababu wewe unaomba ujira. Unafanya haya ukitaka ujira. Hii ndiyo du´aa ya ´ibaadah. Mwenye kuswali, mwenye kuleta Tasbiyh, mwenye kutoa swadaqah, mwenye kuhiji na mwenye kufanya ´Umrah, yote haya ni du´aa ya ´ibaadah. Wameyatenda hayo wakitarajia thawabu kutoka kwa Allaah.

Du´aa ya maombi ni kuomba moja kwa moja:

”Ee Allaah nisamehe! Ee Allaah nirehemu! Ee Allaah niokoe na Moto! Ee Allaah niingize Peponi!”

Hii huitwa du´aa ya maombi. Ni ombi la moja kwa moja.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31696/ما-الفرق-بين-دعاء-العبادة-ودعاء-المسالة
  • Imechapishwa: 15/11/2025