Swali: Kuna baadhi ya mebedui wahamahamaji ambao huenda kuchota maji kutoka umbali wa zaidi ya 80 km, hali ambayo hutokea mara kwa mara. Ni ipi hukumu ya Shari´ah kwao? Je, inajuzu kwao kufupisha swalah? Je, inajuzu pia kwao kufungua swawm katika Ramadhaan, kwa kuwa wanapata uzito katika kufanya hivyo, khaswa wanapokwenda kuchota maji? Kwa mfano huleta maji ndani ya muda wa saa ishirini na nne, kisha hupumzika siku tatu au mbili, halafu huenda tena na kuyachota. Je, inajuzu kwao kufanya Tayammum wakiwa katika hali hii?
Jibu: Kwa wale wanaokwenda kuchota maji, basi inajuzu kufupisha swalah na kufungua swawm katika umbali uliotajwa. Wote wanatakiwa kutawadha kwa kutumia maji waliyoyachota kwa ajili yao na wanyama wao, isipokuwa wakati ambapo maji yanakuwa machache na wanaogopa kwamba wakitawadha kwa kutumia maji hayo wao au wanyama wao watapata madhara. Katika hali hiyo pekee inajuzu kwao kufanya Tayammum.
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/333)
- Imechapishwa: 21/11/2026
Swali: Kuna baadhi ya mebedui wahamahamaji ambao huenda kuchota maji kutoka umbali wa zaidi ya 80 km, hali ambayo hutokea mara kwa mara. Ni ipi hukumu ya Shari´ah kwao? Je, inajuzu kwao kufupisha swalah? Je, inajuzu pia kwao kufungua swawm katika Ramadhaan, kwa kuwa wanapata uzito katika kufanya hivyo, khaswa wanapokwenda kuchota maji? Kwa mfano huleta maji ndani ya muda wa saa ishirini na nne, kisha hupumzika siku tatu au mbili, halafu huenda tena na kuyachota. Je, inajuzu kwao kufanya Tayammum wakiwa katika hali hii?
Jibu: Kwa wale wanaokwenda kuchota maji, basi inajuzu kufupisha swalah na kufungua swawm katika umbali uliotajwa. Wote wanatakiwa kutawadha kwa kutumia maji waliyoyachota kwa ajili yao na wanyama wao, isipokuwa wakati ambapo maji yanakuwa machache na wanaogopa kwamba wakitawadha kwa kutumia maji hayo wao au wanyama wao watapata madhara. Katika hali hiyo pekee inajuzu kwao kufanya Tayammum.
Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/333)
Imechapishwa: 21/11/2026
https://firqatunnajia.com/tayammum-kwa-watu-ambao-wanaenda-kuchota-maji-umbali-wa-zaidi-ya-80-km/