Swali: Sisi ni miongoni mwa wakaazi wa maeneo ya vijijini. Muda wetu wote tunahama kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Tuna magari matatu ya tenki la maji ya kuchota maji kwa ajili yetu, kondoo na ngamia. Sisi ni familia kumi na mbili na magari hayo ya tenki yanamilikiwa na familia tatu, huku wengine wakinywa pamoja nao. Je, inajuzu kwetu kufanya Tayammum badala ya kutawadha? Ikizingatiwa kwamba umbali kutoka kwenye vyanzo vya maji unatofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Jibu: Ikiwa maji yanapatikana kwenu, basi ni wajibu kwenu kujitwaharisha kwa kutumia maji hayo kwa twahara kubwa na ndogo. Ikiwa maji hayapatikani, basi inajuzu kufanya Tayammum pale ambapo maji yako mbali na kuna uzito wa kuyachukua wakati wa swalah.
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/333)
- Imechapishwa: 21/11/2026
Swali: Sisi ni miongoni mwa wakaazi wa maeneo ya vijijini. Muda wetu wote tunahama kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Tuna magari matatu ya tenki la maji ya kuchota maji kwa ajili yetu, kondoo na ngamia. Sisi ni familia kumi na mbili na magari hayo ya tenki yanamilikiwa na familia tatu, huku wengine wakinywa pamoja nao. Je, inajuzu kwetu kufanya Tayammum badala ya kutawadha? Ikizingatiwa kwamba umbali kutoka kwenye vyanzo vya maji unatofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Jibu: Ikiwa maji yanapatikana kwenu, basi ni wajibu kwenu kujitwaharisha kwa kutumia maji hayo kwa twahara kubwa na ndogo. Ikiwa maji hayapatikani, basi inajuzu kufanya Tayammum pale ambapo maji yako mbali na kuna uzito wa kuyachukua wakati wa swalah.
Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/333)
Imechapishwa: 21/11/2026
https://firqatunnajia.com/ni-wajibu-kujitwaharisha-kwa-maji-midhali-mnapata-maji-japo-kwa-taabu/