Swali: Tunaishi maeneo ya vijijini na ninapenda kusoma Qur-aan. Wakati mwingine tunauchukua msahafu ili nisome na kuhifadhi nilichosoma. Lakini wakati mwingine sipati maji na hivyo tunauweka msahafu chini, kisha nafanya Tayammum na kuuchukua msahafu. Je, inajuzu kwa mwenye kufanya Tayammum kuushika msahafu?

Jibu: Ikiwa muislamu hawezi kutumia maji au hajayapata, inajuzu kwake kufanya Tayammum na kuushika msahafu.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/341)
  • Imechapishwa: 22/11/2026