Ni ipi hukumu ya swalah ya Tayammum katika hali hii?

Swali: Wakati wa siku ya masomo, kabla ya swalah ya Dhuhr, maji yaliisha msikitini. Tulijua kwa yakini kwamba kuna maji shuleni, lakini yako nyuma ya mlango uliofungwa ambao haufunguliwi mpaka siku ya masomo itakapomalizika. Pia tunajua kwamba kuna maji nje ya shule katika sehemu iliyo karibu. Ni ipi hukumu ya kufanya Tayammum katika hali hii? Ikizingatiwa kwamba muda wa kumalizika kwa siku ya masomo ni takriban saa moja na nusu kabla ya swalah ya ´Aswr.

Jibu: Kufanya Tayammum hakusihi ikiwa kuna maji yaliyo karibu. Inajuzu kwenu kuchelewesha swalah kutoka mwanzo wa wakati wake na kusubiri maji, maadamu muda wa swalah bado haujaisha.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/342)
  • Imechapishwa: 22/11/2026