Swali: Je, inafaa kufanya Tawassul kwa wafu? Ni ipi hukumu ya anayefanya Tawassul kwa wafu? Ni ipi Tawassul inayokubalika katika Shari´ah?

Jibu: Kufanya Tawassul kwa wafu katika yale wasiyoyaweza… na wao hakuna chochote wanachokiweza. Ni Bid´ah pale ambapo haijafikia katika kiwango cha imani. Tawassul inayokubalika kwa mujibu wa Shari´ah ni ku-Tawassul kwa majina na sifa Zake. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلِلّهِ الأَسْمَاء الْحُسْنَى فَادْعُوهُ بِهَا

”Allaah ana majina mazuri mno; hivyo basi muombeni kwayo.”[1]

Pia inafaa kufanya Tawassul kwa mtu aliye hai katika yale anayoyaweza. Yule bwana kipof ambaye alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema: ”Ee Muhammad! Mimi natawasali kwa du´aa yako mbele ya Mola wangu.” Mtume hapa alikuwa hai na muweza wa kumwombea. Pia inafaa kufanya Tawassul kwa matendo mema, kama ilivyo katika kile kisa cha watu wa pangoni.

[1] 07:180

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 26
  • Imechapishwa: 22/07/2025