Swali: Je, kuna Hadiyth ambazo ni Swahiyh kuhusiana na Safari ya usiku na ya Kupandishwa mbinguni?

Jibu: Haikuthibiti tarehe ya Safari ya usiku na ya Kupandishwa mbinguni, kama alivosema Haafidhw Ibn Hajar katika “Tibyiyn-ul-´Ajab”. Humo anasema kuwa haikuthibiti kwamba Safari ya usiku na ya Kupandishwa mbinguni ilikuwa tarehe 27 Rajab. Kwa mujibu wake ni kwamba wapiga visa ndio hutaja tarehe hiyo kwamba kulitokea tukio hilo. Kisha akasema kuwa hata kama ingelithibiti, basi hatuna ruhusa ya kuzua ´ibaadah ambayo haikuthibiti ndani ya Qur-aan na Sunnah.

Tazama jinsi Suufiyyah wanavojigonga! Upande mmoja wanasema kuwa Hadiyth niyngi kuhusu picha zimesimuliwa na mpokezi mmoja (حديث الآحاد). Upande wa pili hawana dalili yoyote juu ya tarehe hiyo, si Hadiyth iliyosimuliwa na mpokezi mmoja wala kitu kingine. Hakuna kingine wanachofata isipokuwa tu matamanio. Kisha wanaita kusherehekea usiku wa tarehe 27 Rajab, usiku wa kuzaliwa kwake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), usiku wa nusu ya Sha´baan, usiku wa kuhajiri. Ni maneno matupu tu.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 353-354
  • Imechapishwa: 16/06/2025