Takfiyr ya Ahbaash kwa Ibn Taymiyyah na al-Albaaniy

Unajua kuwa hakuna pote wala kundi lolote linalotumikia manufaa ya Uislamu ya kijumla na khaswa manufaa ya Salafiyyah. Utaona msaada unawajia kutoka kila pande. Kipindi cha mwisho tumepewa mtihani na wale wenye kujiita “Ahbaash”.

Watu hawa wana nguvu na mamlaka Lebanon. Wako kama nchi ndani ya nchi. Wana silaha. Wana magari. Wanaua. Wanapiga. Wametawala makumi ya Misikiti Lebanon. Mwishowe wameingia hapa (Jordan) na kupata msaada. Wameanza kuhutubu kwenye Misikiti na wanamkufurisha wazi wazi Shaykh-ul-Islaam na Shaykh al-Albaaniy ambaye bado anaishi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (930)
  • Imechapishwa: 30/08/2020

Turn on/off menu