Takbiyr za pamoja kwenye vipaza sauti

Swali 181: Ni ipi hukumu ya Takbiyr za kwenye vipaza sauti siku ya ´iyd?

Jibu: Watu wanatakiwa kuacha hivo. Takbiyr za pamoja ni Bid´ah.

Swali 182: – Vipi mtu akafanya Takbiyr kwenye vipaza sauti peke yake?

Jibu: Hapana vibaya.

Swali: Lakini watu watafata kipaza sauti na kwa hiyo sauti itakuwa ya pamoja?

Jibu: Anawakumbusha.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 76
  • Imechapishwa: 05/04/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´