Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) amesema katika “al-Minhaaj” (06/293):

“Halafu katika maajabu ni kwamba Raafidhwah wanamkemea ´Uthmaan kitu kilichoshuhudiwa na Answaar na Muhaajiruun na hawakumkemea. Bali waislamu wote wakamfuata juu ya adhaana ya ijumaa.”

al-Hajuuriy hakukomeka katika udhalilifu na aibu hii juu ya haki ya ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh). Bali akataka kuufanyia Tabdiy´ umati mzima unaomfuata ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh). Amesema katika “Ahkaam-ul-Jumu´ah”:

“Ama yule mwenye kumfuata – yaani ´Uthmaan – juu ya kosa hilo baada ya kubainishiwa hoja, basi ni mzushi na hana udhuru wowote katika kwenda kinyume na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake.”[1]

Je, al-Hajuuriy hakujua fadhila za Maswahabah juu ya waumini wote zinazoendelea mpaka siku ya Qiyaamah na kwamba kila kheri ambayo sisi tumo ndani yake basi ni kwa ajili ya baraka za Maswahabah – kwani wao ndio waliotunakilia elimu na Shari´ah.

[1] 315

  • Mhusika: Shaykh ´Arafaat bin Hasan bin Ja´far al-Muhammadiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan al-Fawriy (02/20-21)
  • Imechapishwa: 08/01/2017