Swali: Nimetazama ndani ya Ramadhaan mida ya asubuhi filamu chafu. Je, swawm yangu inazingatiwa ni yenye kukubaliwa?

Jibu: Haijuzu kutazama filamu chafu. Haijalishi kitu ndani ya Ramadhaan wala katika miezi mingine. Ndani ya Ramadhaan dhambi zinakuwa nzito zaidi. Mfungaji akitokwa na manii kwa sababu ya utazamaji huu basi swawm yake inaharibika na atalazimika kulipa siku hii ambayo ametokwa na manii.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

´Abdullaah bin Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

Bakr Abu Zayd

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (09/213) nr. (18622)
  • Imechapishwa: 24/04/2022