Swali: Vipi kuhusu Hadiyth isemayo:
“Swalini swalah ya mwenye kuaga.”?
Jibu: Hadiyth hii haina neno. Hadiyth iliyopokelewa na al-´Irbaadhw ambaye ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaswalisha watu swalah kubwa mno, kana kwamba ni swalah ya mwenye kuaga, kisha akawakhutubu Khutbah yenye nasaha kana kwamba ni nasaha ya mwenye kuaga. Ama lafudhi lenye kusema:
“Swalini swalah ya mwenye kuaga.”
mimi sijui usahihi wa cheni yake, lakini maana yake ni sahihi. Inafaa kwa muumini kila anaposwali ajihisi kana kwamba huenda hii ndiyo swalah yake ya mwisho. Kwa hiyo aiangalie kwa unyenyekevu na ukamilifu.
Swali: Je, imamu anaweza kuwaambia maamuma:
“Swalini swalah ya mwenye kuaga.”
badala ya kusema:
“Simameni sawasawa.”?
Jibu: Sijui kama kuna msingi wa kufanya hivyo. Afanye kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kusema:
”Sawazisheni safu zenu, karibianeni na karibianeni.”
Sijui jambo jipya. Katika yale Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyofanya yanatosheleza.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31145/ما-صحة-حديث-صلوا-صلاة-مودع-وحكم-قولها
- Imechapishwa: 07/10/2025
Swali: Vipi kuhusu Hadiyth isemayo:
“Swalini swalah ya mwenye kuaga.”?
Jibu: Hadiyth hii haina neno. Hadiyth iliyopokelewa na al-´Irbaadhw ambaye ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaswalisha watu swalah kubwa mno, kana kwamba ni swalah ya mwenye kuaga, kisha akawakhutubu Khutbah yenye nasaha kana kwamba ni nasaha ya mwenye kuaga. Ama lafudhi lenye kusema:
“Swalini swalah ya mwenye kuaga.”
mimi sijui usahihi wa cheni yake, lakini maana yake ni sahihi. Inafaa kwa muumini kila anaposwali ajihisi kana kwamba huenda hii ndiyo swalah yake ya mwisho. Kwa hiyo aiangalie kwa unyenyekevu na ukamilifu.
Swali: Je, imamu anaweza kuwaambia maamuma:
“Swalini swalah ya mwenye kuaga.”
badala ya kusema:
“Simameni sawasawa.”?
Jibu: Sijui kama kuna msingi wa kufanya hivyo. Afanye kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kusema:
”Sawazisheni safu zenu, karibianeni na karibianeni.”
Sijui jambo jipya. Katika yale Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyofanya yanatosheleza.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31145/ما-صحة-حديث-صلوا-صلاة-مودع-وحكم-قولها
Imechapishwa: 07/10/2025
https://firqatunnajia.com/swalah-ya-mwenye-kuaga-ii/