Swali: Ni kawaida katika kazi yake kutoa harufu mbaya kama harufu ya samaki. Je, anapewa udhuru wa kuacha swalah ya mkusanyiko kama mlinzi au afanye nini?

Jibu: Ndio, ikiwa anawaudhi watu kwa haarufu yake mbaya. Asiwali pamoja na watu mpaka baada ya kujisafisha.

Swali: Nyakati za swalah zinamjia akiwa yuko kazini na inamtoka harufu mbaya?

Jibu: Akiwa na uwezo wa kuiondosha na kuhudhuria mkusanyiko, hapo itakuwa ni wajibu kwake.

Swali: Asipoweza?

Jibu: Anakuwa kama mfano wa mla kitunguu saumu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23793/حكم-الجماعة-لمن-راىحته-كريهة-بسبب-مهنته
  • Imechapishwa: 04/05/2024