Swalah ya ijumaa kwa wafungwa magerezani

Swali: Mnajua kwamba magereza yanajumuisha kundi kubwa la vijana ambao Allaah amepanga waingie katika mahali hapa pa kutisha. Tunamuomba Allaah Atulinde sisi na nyinyi na shari yake. Lakini tatizo ni kwamba ananieleza mmoja wa ndugu walioingia gereza la al-´Awud kwamba hawatekelezewi swalah miongoni mwao wala polisi hawawaamrishi wafungwa kuswali. Aidha hawatekelezewi swalah ya ijumaa miongoni mwao, hali ya kuwa idadi yao ni kubwa na wanaoswali ni karibu asilimia moja. Ni kwa nini haamrishwi kueneza katika magereza yote ya nchi, kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Ndani, amri ya swalah na kuwaadhibu wasioswali?

Jibu: Kunahitaji kuchunguza vyema juu ya kusihi kwa khabari hii. Bado walinganiaji wanatembelea magereza hapa na katika maeneo ya magharibi na mashariki. Walinganiaji wanawasiliana mara kwa mara, wanawaongoza na kuwafundisha. Haijatufikia kutoka kwao hili alilotaja mwandishi. Lakini tutaangalia jambo hili – Allaah akitaka na tutathibitisha. Ikiwa kuna kitu katika hili, basi ni lazima kuangaliwa jambo la wafungwa na kuwaelekeza kwenye kheri, si kwa upande wa swalah ya mkusanyiko tu wala kwa upande wa swalah ya ijumaa ikiwa inawezekana. Ikiwa haiwezekani, basi wana udhuru. Mfungwa ana udhuru katika swalah ya ijumaa, isipokuwa ikiwa itawezekana kusimamishwa miongoni mwao, basi hili ni jambo jingine.

Hakika imeulizwa kuhusu hilo na wanazuoni wameamua kwamba mfungwa hana uwajibu wa ijumaa; isipokuwa ikiwa itawezekana kuisimamisha na ijumaa ikasimamishwa karibu naye na ikawezekana kuhudhuria kwake au ikasimamishwa gerezani na ikawezekana kuhudhuria, basi katika hali hili likiwezekana linawezekana. Lakini wengi wa wafungwa hawawezi kuhudhuria, kwa sababu wako katika mahali maalum na kuna khofu katika kusogezwa kwao shari au kutoroka. Kwa kifupi ni kwamba hili ni jambo la kuangaliwa katika upande wa swalah ya ijumaa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3506/حكم-اقامة-صلاة-الجمعة-في-السجون
  • Imechapishwa: 18/11/2026

Turn on/off menu