Swali: Hakika kuchanganyika kunatokea na ni jambo lisiloepukika katika shule za msingi na katika taasisi za sekondari na vyuo vikuu katika nchi zisizo hii ambayo Allaah ameihifadhi. Je, msichana muislamu asome ndani ya mazingira haya ambayo yamechanganyika mambo au mnaona aache masomo? Je, katika kuacha kwake elimu kuna upungufu katika haki yake ya elimu ya kidini ili aimarishe imani yake na utamaduni wake wa Kiislamu?
Jibu: Ndiyo, ndiyo. Ikiwa kujifunza kunakuwa kwa kuchanganyika, basi aache elimu na aache kujifunza. Abaki katika nyumba yake na amfundishe baba yake, ndugu yake au mume wake. Asili ya dini na taarifa zinazomlazimu ni chache. Ni rahisi kupatikana nyumbani. Watu wanataka kupanuka ili waajiriwe. Ama kujifunza ”al-Faatihah” na yale yanayowezekana katika Kitabu cha Allaah, kujifunza ´Aqiydah na kujifunza swalah, yote hayo ni mepesi. Ama kwenda kusoma pamoja na vijana kwa kuchanganyika, hapana. Ama ikiwa ni katika chekechea chini ya umri ambao ndani yake kuna fitina na shahawa, chini ya miaka tisa, hili ni kwa ajili ya dharurah, khaswa chini ya miaka saba katika mwanzo wa masomo katika chekechea, jambo lake ni jepesi. Lakini ikiwa mlango utafunguliwa katika msingi, utaendelea hadi shule ya msingi, kisha utaendelea hadi sekondari na hivyo hivyo, jambo ambalo ni balaa kubwa. Lakini kubaki kwake nyumbani na kumfundisha baba yake, mama yake, dada yake au kumletea mwalimu, hata kwa dini, hata kwa mali, basi hili ni bora kwake na linafaa zaidi. Haijuzu kabisa aingie katika hali ya kuchanganyika na vijana.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3494/دراسة-الفتاة-في-المدارس-والجامعات-التي-فيها-اختلاط
- Imechapishwa: 18/11/2026
Swali: Hakika kuchanganyika kunatokea na ni jambo lisiloepukika katika shule za msingi na katika taasisi za sekondari na vyuo vikuu katika nchi zisizo hii ambayo Allaah ameihifadhi. Je, msichana muislamu asome ndani ya mazingira haya ambayo yamechanganyika mambo au mnaona aache masomo? Je, katika kuacha kwake elimu kuna upungufu katika haki yake ya elimu ya kidini ili aimarishe imani yake na utamaduni wake wa Kiislamu?
Jibu: Ndiyo, ndiyo. Ikiwa kujifunza kunakuwa kwa kuchanganyika, basi aache elimu na aache kujifunza. Abaki katika nyumba yake na amfundishe baba yake, ndugu yake au mume wake. Asili ya dini na taarifa zinazomlazimu ni chache. Ni rahisi kupatikana nyumbani. Watu wanataka kupanuka ili waajiriwe. Ama kujifunza ”al-Faatihah” na yale yanayowezekana katika Kitabu cha Allaah, kujifunza ´Aqiydah na kujifunza swalah, yote hayo ni mepesi. Ama kwenda kusoma pamoja na vijana kwa kuchanganyika, hapana. Ama ikiwa ni katika chekechea chini ya umri ambao ndani yake kuna fitina na shahawa, chini ya miaka tisa, hili ni kwa ajili ya dharurah, khaswa chini ya miaka saba katika mwanzo wa masomo katika chekechea, jambo lake ni jepesi. Lakini ikiwa mlango utafunguliwa katika msingi, utaendelea hadi shule ya msingi, kisha utaendelea hadi sekondari na hivyo hivyo, jambo ambalo ni balaa kubwa. Lakini kubaki kwake nyumbani na kumfundisha baba yake, mama yake, dada yake au kumletea mwalimu, hata kwa dini, hata kwa mali, basi hili ni bora kwake na linafaa zaidi. Haijuzu kabisa aingie katika hali ya kuchanganyika na vijana.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3494/دراسة-الفتاة-في-المدارس-والجامعات-التي-فيها-اختلاط
Imechapishwa: 18/11/2026
https://firqatunnajia.com/mwanamke-aendelee-na-masomo-katika-shule-ya-sekondari-iliyo-na-mchanganyiko/