Wanazuoni wamesema kwamba chaguo bora ni kusoma kwa kufuata mpangilio wa msahafu. Kwa msemo mwingine asome al-Faatihah, kisha al-Baqarah, kisha Aal ´Imraan, kisha zinazofuata kwa mpangilio huo, ni mamoja iwe anasoma ndani ya swalah au nje yake. Mpaka wamefikia kusema baadhi ya maswahiba wetu kwamba ikiwa mtu katika Rak´ah ya kwanza atasoma Suurah “an-Naas”, basi katika Rak´ah ya pili asome ”al-Baqarah”.
Baadhi ya maswahiba wetu wamesema kwamba inapendekezwa akisoma Suurah asome inayofuata baada yake. Dalili ya hili ni kuwa mpangilio wa msahafu umewekwa hivyo kwa hekima. Kwa hivyo inatakikana kuulinda, isipokuwa katika yale ambayo Shari´ah imekuja kuyabagua. Mfano wa jambo hilo ni swalah ya Fajr siku ya ijumaa ambapo katika Rak´ah ya kwanza atasoma Suurah ”as-Sajdah” na Rak´ah ya pili atasoma “al-Insaan”. Katika swalah ya ´iyd katika Rak´ah ya kwanza atasoma “Qaaf” na Rak´ah ya pili atasoma “al-Qamar”. Rak´ah mbili za Sunnah ya Fajr ambapo Rak´ah ya kwanza atasoma ”al-Kaafiruun” na Rak´ah ya pili anasoma “al-Ikhlaasw”. Rak´ah za witr ambapo ya kwanza kunasomwa ”al-A´laa”, Rak´ah ya pili kunasomwa “al-Kaafiruun” na Rak´ah ya tatu kunasomwa “al-khlaasw”.
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 62
- Imechapishwa: 18/11/2026
Wanazuoni wamesema kwamba chaguo bora ni kusoma kwa kufuata mpangilio wa msahafu. Kwa msemo mwingine asome al-Faatihah, kisha al-Baqarah, kisha Aal ´Imraan, kisha zinazofuata kwa mpangilio huo, ni mamoja iwe anasoma ndani ya swalah au nje yake. Mpaka wamefikia kusema baadhi ya maswahiba wetu kwamba ikiwa mtu katika Rak´ah ya kwanza atasoma Suurah “an-Naas”, basi katika Rak´ah ya pili asome ”al-Baqarah”.
Baadhi ya maswahiba wetu wamesema kwamba inapendekezwa akisoma Suurah asome inayofuata baada yake. Dalili ya hili ni kuwa mpangilio wa msahafu umewekwa hivyo kwa hekima. Kwa hivyo inatakikana kuulinda, isipokuwa katika yale ambayo Shari´ah imekuja kuyabagua. Mfano wa jambo hilo ni swalah ya Fajr siku ya ijumaa ambapo katika Rak´ah ya kwanza atasoma Suurah ”as-Sajdah” na Rak´ah ya pili atasoma “al-Insaan”. Katika swalah ya ´iyd katika Rak´ah ya kwanza atasoma “Qaaf” na Rak´ah ya pili atasoma “al-Qamar”. Rak´ah mbili za Sunnah ya Fajr ambapo Rak´ah ya kwanza atasoma ”al-Kaafiruun” na Rak´ah ya pili anasoma “al-Ikhlaasw”. Rak´ah za witr ambapo ya kwanza kunasomwa ”al-A´laa”, Rak´ah ya pili kunasomwa “al-Kaafiruun” na Rak´ah ya tatu kunasomwa “al-khlaasw”.
Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 62
Imechapishwa: 18/11/2026
https://firqatunnajia.com/57-bora-ni-kusoma-qur-aan-kwa-mpangilio/