´Ubaadah bin as-Swaamit (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Dhahabu kwa dhahabu, fedha kwa fedha, ngano kwa ngano, shayiri kwa shayiri, tende kwa tende, chumvi kwa chumvi, mfano kwa mfano, sawa kwa sawa. Ikiwa aina hizi zitatofautiana, basi uzeni mnavyotaka ikiwa ni mkono kwa mkono. Yule mwenye kuongeza au kuomba kuongezewa, basi amefanya ribaa.”[1]
Haijuzu kuuza chakula kinachopimwa kwa kipimo au uzito kwa aina yake isipokuwa sawa kwa sawa. Wala haijuzu kuuza kitu kinachopimwa kwa kipimo miongoni mwa hivyo kwa kitu cha aina yake kwa uzito, wala kitu kinachopimwa kwa uzito kwa kipimo. Ikiwa aina hizo mbili zitatofautiana, basi inajuzu kukiuza kwa namna yoyote atakavyo, ikiwa ni mkono kwa mkono. Wala haijuzu kuchelewesha malipo ndani yake, wala kutengana kabla ya kupokeana, isipokuwa katika thamani kwa bidhaa.
Vitu viwili vyovyote vinavyokusanywa na jina maalum, basi ni aina moja, isipokuwa ikiwa vinatokana na asili mbili tofauti. Kwa hiyo matawi ya aina ni aina tofauti, hata kama majina yao yanafanana, kama unga mbalimbali na mafuta mbalimbali.
Wala haijuzu kuuza kilicho kibichi miongoni mwa hivyo kwa kilichokauka cha aina yake, wala kilicho safi kwa kilichochanganywa, wala kibichi kwa kilichopikwa.
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kununua tende zilizo juu ya mitende, lakini ameruhusu matunda ya mtende uliotolewa kuwa zawadi kuuzwa kwa kiasi kisichozidi mizigo mitano ya ngamia, kwa makadirio ya kiasi, ili wenye nayo waweze kuzila zikiwa mchi.
[1] Muslim (1587).
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 53
- Imechapishwa: 18/11/2026

Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 53
Imechapishwa: 18/11/2026
https://firqatunnajia.com/80-ribaa/