Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza ugusaji, ikiwa na maana ya mtu kusema: ´Nguo yoyote nitakayoigusa basi ni yako kwa kiasi fulani.´
Amekataza urushaji, ikiwa na maana ya mtu kusema: ´Nguo yoyote nitakayokutupia basi ni yangu kwa kiasi fulani.´
Amekataza kuuza kwa kurusha jiwe, nako ni mtu kusema: ´Rusha vijiwe hivi; nguo yoyote litakapoangukia basi ni kwa bei kadhaa.`
Amekataza kuuza kwa mtu mwingine juu ya biashara ya ndugu yake.
Amekataza kuuza kwa mtu wa mjini kwa ajili ya mtu wa vijijini, nayo ni kuwa mtu wa mjini awe dalali wake.
Amekataza mtu kuongeza bei ya kuuza bidhaa ilihali yeye hataki kuinunua.
Amekataza biashara mbili ndani ya biashara moja, nayo ni kusema: ´Nimekuuzia hii kwa dirhamu kumi zilizo kamili au ishirini zilizovunjwa.´ Inaweza pia kuwa na maana ya mtu kusema: ´Nimekuuzia hii kwa sharti kwamba uniuzie hii au ununue kutoka kwangu hii.´
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Msipokee bidhaa kabla hazijashushwa sokoni.”[1]
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tena:
“Yule mwenye kununua chakula, basi asikiuze mpaka akipokee kikamilifu.”[2]
[1] al-Bukhaariy (2165) na Muslim (1517).
[2] Muslim (1518).
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 51-52
- Imechapishwa: 18/11/2026
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza ugusaji, ikiwa na maana ya mtu kusema: ´Nguo yoyote nitakayoigusa basi ni yako kwa kiasi fulani.´
Amekataza urushaji, ikiwa na maana ya mtu kusema: ´Nguo yoyote nitakayokutupia basi ni yangu kwa kiasi fulani.´
Amekataza kuuza kwa kurusha jiwe, nako ni mtu kusema: ´Rusha vijiwe hivi; nguo yoyote litakapoangukia basi ni kwa bei kadhaa.`
Amekataza kuuza kwa mtu mwingine juu ya biashara ya ndugu yake.
Amekataza kuuza kwa mtu wa mjini kwa ajili ya mtu wa vijijini, nayo ni kuwa mtu wa mjini awe dalali wake.
Amekataza mtu kuongeza bei ya kuuza bidhaa ilihali yeye hataki kuinunua.
Amekataza biashara mbili ndani ya biashara moja, nayo ni kusema: ´Nimekuuzia hii kwa dirhamu kumi zilizo kamili au ishirini zilizovunjwa.´ Inaweza pia kuwa na maana ya mtu kusema: ´Nimekuuzia hii kwa sharti kwamba uniuzie hii au ununue kutoka kwangu hii.´
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Msipokee bidhaa kabla hazijashushwa sokoni.”[1]
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tena:
“Yule mwenye kununua chakula, basi asikiuze mpaka akipokee kikamilifu.”[2]
[1] al-Bukhaariy (2165) na Muslim (1517).
[2] Muslim (1518).
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 51-52
Imechapishwa: 18/11/2026
https://firqatunnajia.com/79-biashara-zilizoharamishwa-2/