Anachelea kupata dhambi kwa kutokuwa na mawasiliano na mama aliyemyonyesha

Swali: Mama yangu alifariki nikiwa mdogo ambapo akaninyonyesha mwanamke pamoja na msichana wake kwa muda mrefu. Kisha nikasafiri na nikatengana nao zaidi ya miaka kumi na nane. Baada ya kurudi kwangu nikajua kwamba ameolewa na ameishi katika kijiji kingine ambacho sijui mahali pake. Ninatamani kumtembelea, lakini simjui na yeye hanijui kutokana na urefu wa muda niliokaa mbali. Ninaogopa adhabu ya kukata uhusiano wa jamaa. Wazazi wake ni wazee sana. Naomba unieleze ni vipi ninaweza kumtembelea dada yangu? Je, juu yangu kuna dhambi kwa kukatika huku au hapana?

Jibu: Kunyonyesha si uhusiano wa ukoo. Lakini inafaa kumfanyia wema mama aliyekunyonyesha na aheshimiwe. Si uhusiano wa ukoo; hata usipomtembelea wala usipomjia, hakuna ubaya juu yako. Uhusiano wa ukoo ni jamaa wa nasaba kama vile mama yako wa nasaba, mama mdogo, shangazi yako, dada zako na mabinamu zako. Ama mama aliyekunyonyesha, watoto wake na jamaa zake si uhusiano wa ukoo. Bali wao wana haki ya wema kwa kadiri iwezekanavyo kwa kumridhisha na kumfanyia wema. Ukijua mahali pake na ukamtembelea kwa upande wa kuthamini na kukiri wema wake kwako, basi hili ni zuri. Ikiwa si hivyo, halikudhuru. Wala huitwi mwenye kukata uhusiano na si kukata uhusiano wa ukoo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3478/ما-ينبغي-نحو-الاقارب-من-جهة-الرضاعة
  • Imechapishwa: 18/11/2026