Swalah ya ambaye sehemu ya uchi wake iko wazi

Swali: Je, mtu akiona uchi wake wakati wa swalah inabatilika?

Jibu: Hapana, haibatiliki. Lakini inampasa mtu kujitahidi kufunika uchi wake kwa umakini zaidi. Anapaswa kuhakikisha kwamba amefunga vizuri vifungo vya nguo, amepunguza uwazi wa shingo ya nguo au kujifunga kitu juu yake ili kuzuia kuonekana kwa uchi wake. Vinginevyo anapaswa kuwa amevaa suruwali au nguo nyingine chini ya vazi lake ili asionekane akiwa na uchi wa wazi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24795/هل-تبطل-صلاة-من-راى-عورته-وقت-الصلاة
  • Imechapishwa: 15/12/2024