Swalah ndani ya ndege zenye maeneo ya kuswalia

Swali: Baadhi ya ndege zina sehemu maalum za kuswalia na kuna alama inayoonyesha upande wa Qiblah. Mtu anaweza kusimama ndani yake pamoja na wengine. Je, inajuzu kuswali ndani yake swalah ya faradhi, kama ilivyo katika meli?

Jibu: Maadamu anaweza kusimama, basi aswali akiwa amesimama. Ikiwa kuna alama inayoonyesha Qiblah, basi ni vyema na ageuke pamoja na ndege kuelekea upande huo. Asiswali akiwa amekaa muda wa kuwa anaweza kusimama, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Swali ukiwa umesimama; ikiwa huwezi, basi swali ukiwa umekaa.”

Mtu huyu anaweza kusimama.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
  • Imechapishwa: 27/09/2026