Swalah kila baina ya adhaana na Iqaamah kwa msafiri

195 – Nilimuuliza Shaykh wetu: Ujumla wa Hadiyth isemayo:

”Baina ya kila adhaana mbili kuna swalah.”

inamuhusu msafiri pia?

Jibu: Si jambo liko mbali; kama Rak´ah mbili za wudhuu´ ambazo zinatokana na sababu[1].

196 – Akaulizwa tena kuhusu Hadiyth isemayo:

”Baina ya kila adhaana mbili kuna swalah.”?

Jibu: Dhahiri ni kwamba ni kama swalah za Rawaatib. Kwa hiyo haziswaliwi safarini.

[1] Nimemsikia Shaykh wetu Ibn ´Uthaymiyn akisema hapana, kwa sababu ni katika aina ya Rawaatib.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 85
  • Imechapishwa: 19/04/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´