Swalah inatakiwa iwe ya wastani

Swali: Ipi bora zaidi kati ya mawili haya: kurefusha sujuud pamoja na du´aa au kurefusha kisimamo pamoja na kisomo?

Jibu: Swalah inatakiwa iwe ya wastani. Ikiwa atasoma kisomo kirefu, basi na Rukuu´ na Sujuud zake nazo ziwe ndefu, na akifupisha kisomo, basi afupishe pia Rukuu´ na Sujuud ili ziwe karibu kwa urefu. Kama alivosema al-Baraa´ bin ´Aazib:

”Niliswali pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na nikakuta kisimamo chake, Rukuu´ yake, kuinuka kwake baada ya Rukuu´, Sujuud yake na kukaa kwake baina ya sijda mbili ni karibu sawa.”

Kwa maana ya kwamba alikuwa na wastani katika swalah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31207/هل-الافضل-طول-السجود-ام-القيام-والقراءة
  • Imechapishwa: 16/10/2025