Swalah iliyompita mtu inaswaliwa haraka iwezekanavyo

Swali: Mtu akipitwa na swalah kutokana na udhuru. Je, inafaa kuichelewesha baada ya kuondoka udhuru?

Jibu: Haijuzu kwako kuchelewesha swalah nje ya wakati wake ukiondoka udhuru. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kupitikiwa na usingizi au akaisahau swalah, basi aiswali pale atapoikumbuka. Haina kafara nyingine isipokuwa hiyo.”[1]

Amefanya kuwa inakidhiwa pale tu inapokumbukwa. Ukichelewesha zaidi, unapata dhambi.

[1] al-Bukhaariy (597) na Muslim (684).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/224)
  • Imechapishwa: 10/04/2026