Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali ndani ya msikiti wenye kaburi? Je, kuna tofauti kati ya kaburi lililo upande wa Qiblah cha msikiti na kaburi lililo nyuma ya msikiti?

Jibu: Swalah haisihi ndani ya msikiti ulio na kaburi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah amewalaani mayahudi na manaswara. Wameyafanya makaburi ya Mitume wao kuwa ni sehemu ya kuswalia. Zindukeni! Msiyafanye makaburi kuwa ni mahali pa kuswalia. Hakika mimi nakukatazeni na jambo hilo.”

Kwa hivyo swalah haisihi muda wa kuwa kaburi lipo msikitini. Haijalishi kitu liko upande wa Qiblah cha msikiti au nyuma ya msikiti. Lakini swalah ni sahihi yakiwa yako nje ya ukuta wa msikiti.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (23)
  • Imechapishwa: 21/11/2021