Swalah hailipwi ukitoka wakati wake mpaka ufike wakati wake siku ya pili?

Swali: Baadhi ya watu wanasema ikiwa mtu amekosa swalah ya Dhuhr kisha akaikumbuka usiku, basi asilipe isipokuwa wakati wa Dhuhr ukifika?

Jibu: Hapana, ni kosa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kupitikiwa na usingizi au akaisahau swalah, basi aiswali pale atapoikumbuka. Haina kafara nyingine isipokuwa hiyo.”[1]

Hakuna cha kuongezwa baada ya maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Swali: Anajengea hoja kwa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika Allaah anayo matendo ya mchana asiyoyakubali usiku…”?

Jibu: Hapana, maneno haya ni batili. Ni kufananisha visivyofanana. Maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yako wazi:

“Mwenye kupitikiwa na usingizi au akaisahau swalah, basi aiswali pale atapoikumbuka. Haina kafara nyingine isipokuwa hiyo.”

[1]al-Bukhaariy (597) na Muslim (684).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31574/ما-صحة-القول-بقضاء-الصلاة-في-نفس-وقتها
  • Imechapishwa: 07/11/2025