Siwezi kusoma al-Faatihah kwa sababu imamu ananichanganya

Swali: Mimi siwezi kusoma al-Faatihah katika swalah ya kusoma kwa sauti ya juu nikiwa nyuma ya imamu, kwa sababu Imaam huanza kusoma mara moja baada ya al-Faatihah. Katika tabia yangu siwezi kusoma wala kuomba ikiwa kuna mtu anayesoma, kwa sababu hunichanganya. Naomba mwongozo.

Jibu: Ni wajibu kwako kusoma al-Faatihah ikiwa uko nyuma ya imamu katika swalah ya kusoma kwa sauti ya juu na ya kimyakimya, hata kama imamu hatanyamaza katika swalah ya kusoma kwa sauti ya juu. Hilo ni kutokana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna swalah kwa yule ambaye hakusoma Mama wa Qur-aan.”[1]

Ameipoke al-Bukhaariy na Muslim.

Amesema vilevile (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Huenda mnasoma nyuma ya imamu wenu?” Wakasema: ”Ndiyo.” Akasema: “Msifanye hivyo; isipokuwa kwa al-Faatihah ya Kitabu. Kwani hakuna swalah kwa yule ambaye hakuisoma.”[2]

[1] Muslim (394).

[2] Abu Daawuud (823).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/153)
  • Imechapishwa: 06/03/2026