Anayetaka kusoma zaidi kuhusu Qunuut, basi arejee katika “Zaad-ul-Ma´aad” ambayo ash-Shawkaaniy na as-Swan´aaniy wanarejesha vitabu vyao “Nayl-ul-Awtwaar” na “Subulus-us-Salaam”.

Qunuut haitakiwi iwe sababu ya kugombana na kuzozana. Magomvi na mizozo ni jambo linalowafurahisha maadui wa Uislamu. Wakumomunisti wanapenda watu wa misikiti wavutane. Ikiwa Ahl-us-Sunnah wanaweza kuswali kwa mujibu wa Sunnah, wafanye hivo. Kama wanaweza kujenga msikiti wao, wafanye hivo. Kama wanaweza kwenda katika msikiti wa Ahl-us-Sunnah, wafanye hivo. Wasipoweza, waswali na waislamu wengine. Swalah ni sahihi katika hali yoyote, ni mamoja kumesomwa Qunuut au hakukusomwa. Lakini kama Abu Maalik Sa´d bin Twaariq bin Ushaym al-Ashja´iy alivomwambia baba yake:

“Ee baba yangu kipenzi! Uliswali nyuma ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Bakr na ´Umar. Je, walikuwa wakikunuti?” Akasema: “Ee mwanangu kipenzi, ni uzushi.”

Bi maana ni Bid´ah.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 338
  • Imechapishwa: 06/07/2025