Swali: Ni ipi tafsiri ya Kauli Yake (Ta´ala):

إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِندَ اللَّـهِ كَمَثَلِ آدَمَ ۖ خَلَقَهُ مِن تُرَابٍ

“Hakika mfano wa ‘Iysaa kwa Allaah ni kama mfano wa Aadam. Amemuumba kutokana na udongo.” (03:59)

pamoja na kwamba ´Iysaa hakuumbwa kwa udongo?

Jibu: Hapana. Makusudio sio haya kuwa ´Iysaa ni kama mfano wa Aadam kwa kuumbwa kwa udongo. Maana yake ni kuwa Allaah Amemuumba ´Iysaa pasina baba kama jinsi Alivyomuumba Aadam kwa udongo pasina baba wala mama. Je, Yule Aliyemuumba Aadam pasina baba wala mama ni Muweza vilevile wa Kumuumba ´Iysaa kwa mama pasina baba? Ndio. Allaah juu ya kila kitu ni Muweza. Anachotaka ni kuwasimamishia hoja wakadhibishaji wanaosema kuwa haiwezekani ´Iysaa akawa ameumbwa pasina baba. Wanasema kuwa ni mtoto wa Zinaa. Mayahudi wanasema kuwa ni mtoto wa Zinaa. Tunamuomba Allaah afya. Wanamtuhumu Maryam (´alayhas-Salaam) kuwa ni mzinifu kama jinsi Shiy´ah wanavyomtuhumu mama wa waumini ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) kuwa ni mzinifu. Allaah Awalaani. Shiy´ah wana ushabihi na mayahudi. Wanawatuhumu Mitume (´alayhimu-Swalaatu was-Salaam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/hadis-fitan-18-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015