Shaykh Swaalih Aalush-Shaykh kuhusu asiyeswali

Wanachuoni wametofautiana juu ya mtu mwenye kukataa kuswali. Hili ni mbali na yule mwenye kuonelea kuwa sio wajibu kwake, sawa ikiwa ni mtu binafsi au kundi la watu, ni kafiri. Hana haki yoyote na mali na damu yake havilindwi. Lakini yule mwenye kukataa kuswali pamoja na kuwa anaonelea kuwa ni wajibu, huyu ndiye wanachuoni wametofautiana juu yake. Kauli sahihi ni kwamba hauawi kwanza mpaka kiongozi au naibu wake amwambie kutubia. Asubiri mpaka wakati wa Swalah ya pili na amuamrishe mara ya tatu, kisha baada ya hapo [akiendelea kukataa kuswali] ndio auawe hali ya kuwa ni mwenye kuritadi. Hii ndio kauli sahihi.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 174
  • Imechapishwa: 17/05/2020