Swali: Je, shaka ya mwenye kutawadha kuhusu kutokea kwa hadathi, ni mamoja iwe ni mkojo, kinyesi au upepo, inaathiri twahara yake kwa sababu tu ya kutokuwa na uhakika kutokana na twahara yake kudumu kwa muda mrefu, au ikiwa msingi ni twahara, basi asizingatie shaka mpaka awe na yakini kwamba hadathi imetokea na vilevile kinyume chake?

Jibu: Ikiwa mtu yuko katika hali ya twahara kisha akapatwa na shaka kwamba hadathi imemtokea, basi shaka yake haiathiri twahara yake ya awali. Ikiwa mtu yuko katika hali ya hadathi, kisha akapata shaka kwamba ametwaharika au hapana, basi bado yuko katika hali ya hadathi na shaka hiyo haina athari. Hii ni kwa sababu yakini haiondolewi kwa shaka. Msingi ni kuendelea kuwepo kwa hali iliyokuwapo mpaka ithibitike kinyume chake. Katika Hadiyth imekuja ya kwamba mtu mmoja alilalamika kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba mtu huhisi kana kwamba kuna kitu kimemtokea wakati wa swalah, ambapo akasema:

“… asiondoke msikitini mpaka asikie sauti au ahisi harufu.”[1]

Imepokelewa na kikosi cha wapokezi isipokuwa at-Tirmidhiy.

Imekuja katika Hadiyth nyingine isemayo:

“Mmoja wenu anapohisi kitu tumboni mwake, kisha akawa na shaka kwamba, je, kimetoka kwake kitu au hakikutoka, basi asiondoke msikitini mpaka asikie sauti au ahisi harufu.”[2]

Ameipokea Muslim na at-Tirmidhiy.

15/280-181

[1] Muslim (01/190).

[2] Muslim (01/190).

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/280-181)
  • Imechapishwa: 23/11/2026