Kutokana na dalili zilizo wazi na matendo ya Salaf na waliokuja baada yao inapendeza kusoma Qur-aan kwa pamoja. Imesihi kwamba Abu Hurayrah na Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anhumaa) wameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna watu wanaomtaja Allaah isipokuwa Malaika huwazunguka, rehema huwafunika, utulivu hushuka juu yao na Allaah huwataja kwa wale walioko Kwake.”[1]
at-Tirmidhiy amesema kuwa ”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh”.
Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hawakusanyiki watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Allaah wakisoma Kitabu cha Allaah na wakikisomeshana kati yao, isipokuwa hushuka juu yao utulivu, rehema huwafunika, Malaika huwazunguka na Allaah huwataja kwa wale walioko Kwake.”[2]
Ameipokea Muslim na Abu Daawuud kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim.
Mu´aawiyah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alijitokeza katika duara la Maswahabah wake akasema: “Ni nini kimewafanya mketi?” Wakasema: ”Tumeketi tukimtaja Allaah na kumshukuru kwa kutuongoza katika Uislamu.” Ndipo akasema: “Amenijia Jibriyl (´alayhis-salaam) akanieleza kuwa Allaah (Ta´ala) anajivunia juu yenu mbele ya Malaika.”[3]
Ameipokea at-Tirmidhiy na an-Nasaa´iy. at-Tirmidhiy amesema:
”Hadiyth ni nzuri na ngeni. Hatujui kuwa imepokelewa kwa njia nyingine isipokuwa hii.”
Zipo Hadiyth nyingi mfano wa hii.
[1] Muslim (2700), at-Tirmidhiy (3378), Ibn Maajah (3791) na Ibn Hibbaan (855).
[2] Muslim (2699), Abu Daawuud (1455 na 4946), at-Tirmidhiy (1425 och 2945), Ibn Maajah (225) na Ibn Hibbaan (768).
[3] Muslim (2701), at-Tirmidhiy (3379), an-Nasaa’iy (5426) na Ibn Hibbaan (813).
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 64
- Imechapishwa: 23/11/2026

Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 64
Imechapishwa: 23/11/2026
https://firqatunnajia.com/60-inapendeza-kusoma-qur-aan-kwa-pamoja/