Kusoma Qur-aan kwa kuangalia msahafu ni bora zaidi kuliko kusoma kwa kuhifadhi, kwa sababu kuangalia msahafu ni ´ibaadah inayotakiwa. Kwa hivyo hukusanyika kusoma na kuangalia. Hivi ndivyo walivyosema swahiba wetu al-Qaadhwiy Husayn, Abu Haamid al-Ghazaaliy (Rahimahu Allaah) pamoja na kikundi katika Salaf.
al-Ghazaaliy amenukuu katika kitabu chake “Ihyaa’ ´Uluum-id-Diyn” kwamba wengi miongoni mwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa wakisoma kutoka ndani ya msahafu na walichukia kupita siku bila kuangalia ndani ya msahafu. Ibn Abiy Daawuud amepokea kuhusu kusoma kwa kuangalia ndani ya msahafu kutoka kwa wengi miongoni mwa Salaf na hakukuonekana tofauti ndani yake. Hata hivyo yangelikuwa maoni mazuri kusema kwamba jambo hili linatofautiana kulingana na watu; yule ambaye unyenyekevu na tafakuri yake vinalingana katika hali ya kusoma kwa kuangalia na kwa kuhifadhi, basi atasoma kwa kuangalia ndani ya msahafu. Na yule ambaye unyenyekevu na tafakuri yake vina nguvu, atasoma kwa kuhifadhi. Lililo dhahiri ni kwamba maneno na matendo ya Salaf yanafasiriwa kwa mujibu wa ufafanuzi huu.
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 63
- Imechapishwa: 23/11/2026
Kusoma Qur-aan kwa kuangalia msahafu ni bora zaidi kuliko kusoma kwa kuhifadhi, kwa sababu kuangalia msahafu ni ´ibaadah inayotakiwa. Kwa hivyo hukusanyika kusoma na kuangalia. Hivi ndivyo walivyosema swahiba wetu al-Qaadhwiy Husayn, Abu Haamid al-Ghazaaliy (Rahimahu Allaah) pamoja na kikundi katika Salaf.
al-Ghazaaliy amenukuu katika kitabu chake “Ihyaa’ ´Uluum-id-Diyn” kwamba wengi miongoni mwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa wakisoma kutoka ndani ya msahafu na walichukia kupita siku bila kuangalia ndani ya msahafu. Ibn Abiy Daawuud amepokea kuhusu kusoma kwa kuangalia ndani ya msahafu kutoka kwa wengi miongoni mwa Salaf na hakukuonekana tofauti ndani yake. Hata hivyo yangelikuwa maoni mazuri kusema kwamba jambo hili linatofautiana kulingana na watu; yule ambaye unyenyekevu na tafakuri yake vinalingana katika hali ya kusoma kwa kuangalia na kwa kuhifadhi, basi atasoma kwa kuangalia ndani ya msahafu. Na yule ambaye unyenyekevu na tafakuri yake vina nguvu, atasoma kwa kuhifadhi. Lililo dhahiri ni kwamba maneno na matendo ya Salaf yanafasiriwa kwa mujibu wa ufafanuzi huu.
Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 63
Imechapishwa: 23/11/2026
https://firqatunnajia.com/59-kusoma-qur-aan-kwa-kuangalia-na-kwa-kuhifadhi/