Ataoga mara ngapi aliyefanya zaidi ya jimaa moja?

Swali: Ikiwa mwanaume atajamiiana na mke wake na nguo pamoja na kitanda vikachafuka kutokana na athari za kujamiiana, je, ni ipi hukumu ya jambo hilo? Je, ni wajibu kwa mwanaume kuoga baada ya kila kujamiiana?

Jibu: Mosi ni kwamba ni wajibu kwake kuosha sehemu za nguo na kitanda zilizopatwa na athari za kujamiiana, kwa sababu huwa na majimaji na unyevunyevu wa tupu unaochanganyika na manii.

Pili ni kwamba ikiwa kichwa cha dhakari ya mwanaume kitaingia katika uke wa mwanamke, basi ni wajibu kuoga josho hata kama manii hayakutoka. Josho moja linatosheleza kwa kujamiiana mara mbili au zaidi, ni mamoja iwe na mke mmoja au wake zaidi. Hii ni kutokana na ilivyothibiti kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwazungukia wake zake kwa josho moja[1].

Imepokelewa na Muslim na watunzi wa Sunan.

Imekuja katika riwaya ya Ahmad na an-Nasaa’iy:

”… katika usiku mmoja kwa josho moja.”[2]

[1] Ahmad (03/225), Muslim (01/171), Abu Daawuud (01/56), an-Nasaa´iy (01/144) na Ibn Maajah (01/194).

[2] Ahmad (03/166), an-Nasaa´iy (01/143) na Ibn Maajah (01/194).

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/293)
  • Imechapishwa: 23/11/2026